Zakitaani Blog

Friday, June 8, 2012

ALIE FUNIKA KWA RASTA NDEFU MORO

MTU mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Rasta Shomari ambaye anaamini ndiye Rasta mwenye
nywele ndefu kuliko wote mkoani Morogoro,jana alikuwa kivutio kwenye ligi ya mchangani
inayoendela kwenye uwanja wa Saba Saba mjini hapa.


Rasta Shomari ambaye ni shabiki mkubwa wa timu ya wapiga debe wa stendi kuu ya Msamvu
inayojulikana na jina la Msamvu Terminal 'Mpira Pesa' ambayo hukodi wachezaji nyota wa timu
kubwa za Dar es Salaam zikiwemo Simba na Yanga, jana aliwaongoza mashabiki wenzake kuisapoti
timu hiyo ya wapiga debe.


Akizungumza na matandao huu, Rasta huyo alisema ana zaidi ya miaka 10 hajazikata nywele hizo, na
alipoulizwa anatumia dawa gani kuziosha alisema ni sabuni ya unga pekee anayoitumia kila
anapooga.


Katika mchezo huo timu hiyo ya wapiga debe iliichapa timu ya Black Viba kwa jumla ya magoli 3-1
ambapo kwa sasa inaongoza kwenye kundi A kwa kuwa na jumla ya pointi 6 ikishinda michezo yote
miwili iliyocheza.

No comments:

Post a Comment