HUSSEIN RAMADHANI(Sharomilionea) amefariki dunia kwa ajali mbaya ya gari
Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo
Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa
mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa
jina la Hussein Ramadhani au SharoMilionea akiwa anaendesha gari namba
T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika
eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na
kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali
Teule ya wilaya ya Muheza” Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala
ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati
ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu
haitembei. Kwenye gari alikua mwenyewe...!!
Hili ndilo gali la sharo milionea alilo kua akiendesha mpaka mauti kumkuta....
liliacha njia na kuingia porini bila kupata pancha wala tair kupasuka...!!
Mwili wa sharomilionea akiwa amekwisha tangulia mbele za haki.. mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi...!!
No comments:
Post a Comment