Zakitaani Blog

Thursday, February 21, 2013

HARUSI ZA KITAA

kamera ya Zakitaani Blog imenasa tukio la harusi ambayo usafiri ulotumika kubeba bwana na bibi harusi  ni bodaboda mkoani lindi kijiji cha mohoro...!! hizi ndo tetesi za kitaani...!!

Wednesday, February 13, 2013

NDUGAI ATUPIWA MATUSI KWENYE SIMU....!!

naibu spika akiongea na waheshimiwa wabungu ndani ya bunge...!!
 
Naibu spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema kuwa hatua ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoa simu yake kwa wananchi kumemuathiri kwa kuwa amekuwa akitukanwa.

Ndugai amesema kuwa watu kadhaa wamemtumia ujumbe mfupi (SMS) ama kumpigia simu za mkononi na kumtukana baada ya Chadema kuwapa simu zake Jumapili iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya viwanja vya Bunge jana, Ndugai alisema amekuwa akitukanwa na baadhi ya watu baada ya chama hicho kuzitamka hadharani.

“Nimejibu simu za mkononi nilizokuwa nikipigiwa na kutukanwa na hata ujumbe mfupi nao nimejibu wakinitukana. Mimi ninajibu kistaarabu kwa kuwa mimi ni kiongozi, siwezi kutoa maneno machafu,” alisema.

Hata hivyo, Ndugai alisema kuwa ugawaji wa namba za simu za mkononi huo unaingilia uhuru wa mtu binafsi. Alisema suala hilo litafanya baadhi ya watu kuathirika kwa kuwa wakati mwingine imemlazimisha kuacha kupokea simu kwa kuwa anadhani ni wale wale ambao wanataka kumtukana.

Jumapili iliyopita, Chadema kilifanya maandamano jijini Dar es Salaam ya kuwapokea wabunge wake kutoka mjini hapa kuhudhuria mkutano wa Kumi wa Bunge na kuhitimisha kwa kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Temeke mwisho.

Katika mkutano huo, viongozi wa chama hicho waliwapatia wananchi waliohudhuria namba za simu za mkononi za Spika wa Bunge, Anne Makinda, na Ndugai, ili kuwashinikiza wang’oke wenyewe kwa madai ya kushindwa kuliongoza Bunge kwa kupendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuukandamiza Upinzani.

Hoja yao kubwa ni kiti cha Spika kukalia rufani takribani 10 bila kuzitolea maamuzi na kutupa hoja binafsi za wabunge wa Upinzani.

Tayari Spika Makinda amepokea simu 200 na sms 400 ambazo zilikuwa zikimtukana.

AJALI MBAYA YA GARI

Watu wanane wamefariki dunia wakiwamo wanafunzi wanne wa shule ya sekondari na watatu kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Mark II kugongana na Mitsubishi Fuso eneo la Chalinze, mkoani Pwani.


Katika ajali hiyo iliyotokea juzi saa 12:00 jioni katika Kitongoji cha Kibiti Tarafa ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Mark II hiyo

yenye namba za usajili T. 363 AZG, iligongana uso kwa uso na Fuso yenye namba za usajili T. 433 AYQ.


Ajali hiyo ilitokea wakati Mark II iliyokuwa ikiendeshwa na Abuu Ahmed (21), kuwa katika mwendo kasi ikitokea Tanga kuelekea Morogoro kujaribu kulipita Fuso lililokuwa likitoka Morogoro kuelekea Dar es Salaam likiendeshwa na Mweta Daniel.


Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Gregory Mushi, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa waliokufa katika ajali hiyo ni wanafunzi wanne wa Shule ya Sekondari Chalinze wote wakazi wa eneo la Msolwa.


Aliwataja kuwa ni Essau Enos (16) wa kidato cha tatu, Latifa Shabani (17), wa kidato cha nne, Bahati George (18), wa kidato cha nne na Stella Isaack Kazimoto, (18).


Aliwataja watu wengine waliofariki dunia wakiwa katika Mark II kuwa ni Hassan Kulunga na Maria Sadick, wakazi wa Ubena ambao umri wao haukufahamika mara moja. Wengine ni dereva wa Mark II, Abuu Ahmed (21) na mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka minne na mitatu aliyefahamika kwa jina la Samwel Ismail, ambaye ni mtoto wa marehemu, Maria Sadick. Aidha, Kaimu Kamanda huyo aliwataja majeruhi waliokuwa wamepanda Fuso kuwa ni William Thobias (30), mkazi wa Matombo mkoani Morogoro na utingo, Ahamad Juma (36).


Mushi alisema majeruhi hao wanaendelea na matibabu katika kituo cha afya Chalinze na miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Tumbi wilayani Kibaha. Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Tumbi, Rose Mtei, alithibitisha kupokea miili minane iliyokuwa imeharibika.


Kufuatia ajali hiyo, Kamanda Mushi ametoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazotokea kwa uzembe na kwamba Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani litawachukulia sheria kali madereva hao.


Shuhuda wa ajali hiyo, Godfrey Bonny, alisema ajali hiyo ilitokea wakati dereva wa Mark II akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake ndipo gari lake lilipokutana uso kwa uso na Fuso.


“Mimi ni mkazi wa Chalinze, ilikuwa ni saa 12:30 jioni, nilisikia kishindo kikubwa na ndipo tulipokwenda katika eneo la tukio na kukuta gari dogo limeharibika vibaya na ikiwa chini ya uvungu wa gari kubwa. Lakini kutokana na kuchelewa kwa Kikosi cha Uokoaji, watu waliokuwamo ndani walipoteza maisha kwa kukosa msaada wa haraka,” alisema Bonny.


Shuhuda mwingine, Yusuph Mjema, ambaye pia ni mkazi wa Chalinze, alisema alipofika eneo la tukio, alikuta watu hao wamebanwa, lakini kutokana na kukosa vifaa maalum kwa ajili ya uokoaji, ilichukua muda mrefu kuwatoa.

Thursday, January 24, 2013

TUMCHANGIE HANIFA AWEZE KUPONA

WANADAMU WENYE ROHO ZA UBINADAMU TUOKOE MAISHA YA HANIFA MWEYE MIAKA 5 TU...!!
Mtoto Hanifa Salum Hassan mwenye umri wa miaka mitano anasumbuliwa na ugonjwa wa Saratani ya Damu (Leukemia) ambao umemfanya ashindwe kusimama na kutembea, anasumbuliwa na maumivu ya kichwa wakati wote, wakati mwingine hushindwa kupumua hivyo kulazimika kupumua kwa kutumia mashine pia hawezi kula analishwa kwa kutumia mirija na pia kila baada ya muda inabidi abadilishiwe damu.
 

 MATIBABU
Matibabu ya mtoto Hanifa ni ya gharama kubwa sana. Ugonjwa wake haukujulikana alipopelekwa Hospitali ya taifa Muhimbili lakini alipopelekwa nchini India gharama za uchunguzi pekee zilikuwa dola 7,600 ambapo mtoto Hanifa aligundulika kuwa na ugonjwa wa Acute lymphoblastic Leukemia. Matibabu yake yalipangwa yawe kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza ya matibabu iligharimu dola 10,000. Mwisho wa awamu ya kwanza zilihitajika dola 10,000 zingine ili aingie kwenye awamu ya pili ya matibabu lakini uwezo wa ndugu na jamaa ulikuwa ndio umeishia hapo hivyo matibabu ya mtoto Hanifa yalilazimika kukatishwa na Hanifa kurudishwa Tanzania. Ripoti za madaktari India zilipelekwa Muhimbili ambapo matibabu ya mtoto Hanifa yalipangwa kugharimu Tsh. milioni 2 kwa mwezi. Hakuna pesa za kumwezesha mtoto kuanza matibabu Muhimbili hivyo mtoto Hanifa amebaki nyumbani jijini Dar es Salaam akiwa kwenye hatari kubwa ya maambukizi mbalimbali ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yake.
Hadi sasa ndugu na jamaa wanahaha kutafuta pesa za kumwezesha mtoto Hanifa kumalizia awamu mbili za matibabu yake nchini India kama ikiwezekana au ikishindikana basi aweze kuanza matibabu Muhimbili.

MICHANGO
Kwa watakaopenda kujitolea kuokoa maisha ya Mtoto Hanifa wanaombwa watoe michango yao kupitia akaunti hizi


Kwa walio Tanzania
Jokha Khamis Issa
Akaunti Namba: 041212000428
People Bank of Zanzibar
Kwa mawasiliano namba ya simu ni: +255 777 462587


Kwa walio nje ya Tanzania wanaweza kutuma michango yao kwa akaunti hii
Suleiman Maadini
Account Number: 15092968
Sort Code: 30-67-99
Bank: Lloyds TSB
Country: United Kingdom
Kwa mawasiliano na Bwana Maadini: +44 78 18674305

Wednesday, January 2, 2013

SAJUKI KUAGA DUNIA

SAJUKI AAGA DUNIA
Huyu ndie sajuki enzi za uhai wake akiwa amekwisha anza kuugua...!!

huyu ndie sajuki akiwa na mkewe wastara.....!!

sajuki ameaga dunia leo asubui zakitaani tunatoa pole kwa familia ya sajuki na waigizaji wote. mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi..
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Apumzike kwa amani kipenzi cha wengi sajuki...!!