Zakitaani Blog

Wednesday, February 13, 2013

NDUGAI ATUPIWA MATUSI KWENYE SIMU....!!

naibu spika akiongea na waheshimiwa wabungu ndani ya bunge...!!
 
Naibu spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema kuwa hatua ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoa simu yake kwa wananchi kumemuathiri kwa kuwa amekuwa akitukanwa.

Ndugai amesema kuwa watu kadhaa wamemtumia ujumbe mfupi (SMS) ama kumpigia simu za mkononi na kumtukana baada ya Chadema kuwapa simu zake Jumapili iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya viwanja vya Bunge jana, Ndugai alisema amekuwa akitukanwa na baadhi ya watu baada ya chama hicho kuzitamka hadharani.

“Nimejibu simu za mkononi nilizokuwa nikipigiwa na kutukanwa na hata ujumbe mfupi nao nimejibu wakinitukana. Mimi ninajibu kistaarabu kwa kuwa mimi ni kiongozi, siwezi kutoa maneno machafu,” alisema.

Hata hivyo, Ndugai alisema kuwa ugawaji wa namba za simu za mkononi huo unaingilia uhuru wa mtu binafsi. Alisema suala hilo litafanya baadhi ya watu kuathirika kwa kuwa wakati mwingine imemlazimisha kuacha kupokea simu kwa kuwa anadhani ni wale wale ambao wanataka kumtukana.

Jumapili iliyopita, Chadema kilifanya maandamano jijini Dar es Salaam ya kuwapokea wabunge wake kutoka mjini hapa kuhudhuria mkutano wa Kumi wa Bunge na kuhitimisha kwa kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Temeke mwisho.

Katika mkutano huo, viongozi wa chama hicho waliwapatia wananchi waliohudhuria namba za simu za mkononi za Spika wa Bunge, Anne Makinda, na Ndugai, ili kuwashinikiza wang’oke wenyewe kwa madai ya kushindwa kuliongoza Bunge kwa kupendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuukandamiza Upinzani.

Hoja yao kubwa ni kiti cha Spika kukalia rufani takribani 10 bila kuzitolea maamuzi na kutupa hoja binafsi za wabunge wa Upinzani.

Tayari Spika Makinda amepokea simu 200 na sms 400 ambazo zilikuwa zikimtukana.

No comments:

Post a Comment