Zakitaani Blog

Tuesday, May 29, 2012

SHANGWE ZA SKONGA.

Ebana juzkati pande za A-town kulkua na kijipati flani katika shule moja pande za sinon, yani wanafunzi walkula bata ile mbaya manake kulkua na misosi kibao na vinyaji vya kutosha pia walipata nafasi ya kubadilishana mawazo na wanafunzi wengine kutoka shule zingine zilizokua zimealikwa....!!
Kama unavyo jua wanafuzi wakishakua pamoja ata akili pia huendana,wtu walipiga vyoda na misosi mpaka wakasaza, haikua misosi ya ajabu ila ni ileile misosi yetu ya kwenye sherehe namanisha wali mchafu au pilau kama tulivyozoea na hakukua na kilevi ni mwendo wa soda moto si unajua tena kiskongaskonga...!!!
Wanafunzi hao walipiga picha za pamoja kwa ukumbusho baadaya kumaliza msosi, na pia walibadilishana namba za simu kwaajili ya mawasiliano zaidi, sijajua ni kwanini asilimia kubwa ya watoto wa kiume walibadilishana namba na watoto wa kike daah..!! ya chini ya kapeti tuyaache hukohuko. 





Pamoja na yote pia kulikua na burudani kama maigizo, ngonjera,nyimbo na washkaji pia walichana...!!
Kikawaida tumezoea kuona watoto wa kike wanakula kwa pozi, msosi kidogo anadai kashiba, ila hapa imekua tofauti kidogo watoto wakike wamepiga msosi bila hata kuona aibu saani full mpaka juu adi mlima na mwisho wa siku kitu kikafutika, kwa maojiano walidai kujivunga sio ishu manake usiposhiba asala kwako...!!




Masela pia hawakubaki nyuma walipiga msosi mpaka kikaeleweka kama unvyomuona mshkaj na kidishi cha msosi....!! 
Kiukweli sherehe ilikua nzuri wtu walikula bata kama kawa...!! izo ndo sherehe za shule zetu za kitaa....!!!

No comments:

Post a Comment