Zakitaani Blog

Thursday, June 7, 2012

MTOTO MWENYE VICHWA VIWILI


Mtoto wa ajabu amezaliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akiwa na vichwa viwili, lakini kiwiliwili chake kikiwa na viungo vya kawaida.

Habari zilizopatikana hospitalini hapo, zinaeleza kuwa, mtoto huyo alizaliwa usiku wa kuamkia jana tarehe 6/6/2012 akiwa na uzito wa kilo 3.5 na mwanamke mmoja ambaye jina lake hakupenda lijulikane ambae ndie mama mzazi wa mtoto huyo...!!

 Taarifa hizo zilisema kuwa, mara baada ya mtoto huyo kuzaliwa, wakunga waliokuwa wakimzalisha mwanamke huyo walishangaa kuona mtoto huyo akiwa na vichwa viwili vilivyoungana katika kiwiliwili cha mwili mmoja. kiukweli ni habari ya maajabu ila tumuombee kwa Mungu....!!

2 comments: