Baada ya kufanya vyema hapa bongo, msanii Aslay Isihaka maarufu kama 'Dogo Aslay' anatarajiwa kuvuka mpaka hadi kwa watani wetu nchini Kenya atakapoenda kugonga show moja jijini Nairobi akisindikizwa na kundi la TMK Wanaume Family.
Meneja wa msanii huyo, Said Fella maarufu kama'Mkubwa Fella' alisema Aslay na kundi la TMK wataondoka bongo leo kuelekea huko kwa ajili ya kuwahi onyesho hilo litakalofanyika kesho kwenye ukumbi wa M.K.U ktk onyesho lifahamikalo kama 'EA Mseto Campus Tour'.
Mkubwa Fella, alisema katika onyesho hilo Dogo Aslay atatambulisha albamu yake mpya ya 'Naenda Kusema' aliyoizundua jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita sambamba na kitabu na filamu, huku TMK Wanaume nao wakigonga nyimbo zao mpya na za zamani.
Fella aliongeza hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa msanii huyo chipukizi kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya kutoa burudani tangu alipomuibua kupitia kituo chake cha Mkubwa na Wanae.
Na pia kundi lote la wanaume family watafanya ngoma na baazi ya wasanii wa kenya, kama vile Nonini, na wengine wakali...! Tuzidi tu kuwaombea mema wasanii wetu wa bongo na sio kuwakandamiza....!!
No comments:
Post a Comment