Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Rais wa lebo ya Sharobaro
Records ya jijini Dar es Salaam, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ kufunga pingu
za maisha, kimwana anayetarajiwa kupika mahajumuti nyumbani kwa bosi
huyo wa wasafi dunia nzima amejulikana.
Kwa mujibu wa habari kutoka chanzo kimoja kilichopo mjini Zanzibar,
kimeidokeza Zakitaani Blog pamoja na Teentz.com kuwa Bob Junior huenda akafunga pingu za maisha
na nyota wa filamu kutoka visiwani humo Halima Ally ‘Imma’ ambaye kwa
kipindi kirefu amekuwa karibu kwa kiasi kikubwa na Produza huyo kila
anaikanyaga ardhi ya visiwa hivyo vya karafuu.
Hakuna mwingine ni Halima, siku zote Bob junior amekuwa akija huku na
tunawaona wakitumia muda mwigi wakiwa pamoja hivyo ni uhakika kuwa
Halima ndiye anayeolewa, na hapo kabla mwenyewe aliwahi kutuambia kuwa
wakati wowote atakuwa mke wa mtu” kilisema chanzo hicho na kuongeza kuwa
kuna wakati mrembo huyo aliwahi kuishi nyumbani kwa akina Bob Junior
kwa majuma kadhaa.
Halima alikuwa mmoja wa mastaa walioshiriki filamu ya Royal Prince
iliyotayarishwa visiwani humo chini ya kampuni kubwa El- Fahad
Production anatariwa kutambulishwa rasmi kama mke wa Bob Junior mbele ya
mashabiki wakati bosi huyo wa Sharabaro atakapokuwa anafanya uzinduzi
wa albamu yake ndani ya Club Billicannas jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment