Zakitaani Blog

Friday, July 20, 2012

NDEGE YA ATC KUPASUKA KIOO

Habari za uhakika zinadai kuwa ndege ya ATCL namba TC 100 ambayo ilikuwa imeondoka Dar mapema asubuhi ya juzi (July 18) kuelekea Mwanza ikipitia KIA imepasuka kioo.

Taarifa zimedai kuwa kioo hicho kilipasuka wakati ndege hiyo ikijiandaa kwenda Mwanza baada ya kuwa imeshatua KIA. Kioo kilichopasuka ni kile cha pembeni kwa rubani upande wa kushoto kwa mujibu wa vyanzo.

Kutokana na tukio hilo ndege hiyo ilizuiwa kuruka hadi pale marekebisho ya kioo hicho yangefanyika. Haijajulikana iwapo imesharuhusiwa ama bado

No comments:

Post a Comment